Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akiwa
na vikosi vya ulinzi na usalama vinavyotoa ulinzi katika msitu wa
Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri alifanya ziara ya
kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu wanaohofiwa
majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya
Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Kushoto ni Mkuu wa Kikosi
Maalum kutoka Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam,
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, William Mwampagale.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akichungulia
pango lililopo katika msitu wa Mapangopori ya Amboni linalodaiwa kuwa ni
njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika
Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini
Tanga.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoa
maelekezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Leonard Paulo (kulia),
mara baada ya kutoka ndani ya pango lililopo katika msitu wa Mapangopori
ya Amboni linalodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa majambazi
waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa
ya Chumbageni, jijini Tanga. Katikati ni Mkuu wa Kikosi Maalum kutoka
Kikosi cha Kutuliza Ghasia Makao Makuu Dar es Salaam, Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi, William Mwampagale.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto meza
kuu) akizungumza katika Kikao cha Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama
kilichofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga. Kulia meza kuu ni
Mkuu wa Mkoa huo, Martine Shigella. Watatu kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta
Jenerali, Ernest Mangu (wapili kushoto). Viongozi hao wamekutana mkoani humo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi na usalama mkoani Tanga.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto)
akimsalimia Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella kabla ya kwenda
katika msitu wa Mapangopori ya Amboni mkoani Tanga. Naibu Waziri
alifanya ziara ya kutembelea mapango hayo ambayo yalikuwa makazi ya watu
wanaohofiwa majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini,
Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, jijini Tanga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI.