Mtu mmoja aliyefahamika kwa Jina la Ibrahim Kiliaki amefariki dunia na
wengine wawili kujeruhiwa vibaya kwenye ajali iliyohusisha magari mawili
kugongana eneo la Mchinga Moja Mkoani Lindi.
Akizungumza na safari redio kamanda wa polisi Mkoani Lindi Renata Mzinga amesema ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali hiyo ambayo ilihusisha gari aina ya fusso na gari ndogo aina ya Range Rover yenye namba za usajili T 777 BTZ kugongana uso kwa uso, huku akidai kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijabainika.
Hata hivyo
kamanda Mzinga amesema majeruhi wa ajali hiyo walikimbizwa katika
hospitali ya Nyangao Mkoani Lindi kwa ajili ya matibabu huku mwili wa
marehemu ukihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti wakisuburi
ndugu jamaa na marafiki kwenda kuuchukua kwaajili ya taratibu za mazishi
na majeruhi wa ajali hali zao zinaendelea vizuri.
Aidha kamanda Mzinga ametoa rai kwa waendeshaji wa vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa pamoja na kuendesha kwa tahadhari hasa nyakati za usiku.