Mauaji ya Kinyama yatokea tena Ujuni Makete, Soma na sikiliza sauti hapa (Audio)

Hatimaye mwili wa kijana Eliudi Mahenge mkazi wa kijiji cha Ujuni kata ya Kitulo wilayani Makete mkoani Njombe ambaye ameuwa kikatili kwa kukatwakatwa na kitu chenye ncha kali na kutupwa shambani umezikwa jana kijijini hapo

Tukio la kuuawa kwake limetokea majira ya saa mbili usiku wa kuamkia jana kijijini hapo huku taarifa za awali zikionesha kuwa mauaji hayo yamesababishwa na wivu wa kimapenzi na mtuhumiwa wa mauaji akitajwa kuwa ni Bw. Nipe Ngogo ambaye amekimbilia kusikojulikana baada a tukio hilo
mwili ukienda kuzikwa.
Bw. Masini Anatory ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Makete ambaye ameufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ametaja sababu zilizopelekea kifo cha marehemu Eliudi Mahenge

Awali kabla ya mwili wa marehemu kwenda kuzikwa Afisa Mtendaji wa kata ya Kitulo Bw Christopher Fungo amelaani mauaji hayo na kusema si tu yanatia hofu wananchi lakini pia yanakwamisha shughuli za kila siku za watu kwa sababu ambazo zingeepukika


Diwani wa kata ya Kitulo Mh Asifiwe Mahenge amewaasa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi lakini pia wawe na tabia ya kutoa taarifa pale wanapohisi kuna ishara za migogoro ya wivu wa kimapenzi ili hatua za kusuluhisha zipatikane mapema kuepuka madhara kama hayo 


Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wetu wakatoa maoni yao kuhusu tukio hilo la kusikitisha
Kiongozi wa msafara wa jeshi la Polisi wilaya ya Makete baada ya kuchukua taarifa zote kuhusu mauaji hayo akapata nafasi ya kuzungumza na wananchi waliofika katika eneo la tukio, na kuwasihi kushirikiana kumtafuta mtuhumiwa wa mauaji hayo, huku akiwasihi wananchi endapo watamkamata wamfikishe kwenye vyombo vya sheria ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi yake


Hadi sasa tayari tukio hilo limeripotiwa kwa jeshi la polisi wilaya ya Makete kwa hatua zaidi za kisheria

Kuona picha zote za tukio hilo Bonyeza hapa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo