Diwani wa Makete ajishindia Pikipiki

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete ambaye pia ni diwani wa kata ya Tandala Mh EGNATIO MTAWA ameshinda tuzo ya pikipiki moja  baada ya kata yake ya Tandala kufanya vizuri katika zoezi la kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF. Mh EGNATIO MTAWA

Tuzo hiyo imetolewa Kufutia ahadi iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi kuwa kata itakayoongoza kwa kaya zake kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF itapewa zawadi ya tuzo ya pikipiki na kwa mkoa wa Njombe zawadi hiyo imekwenda kwa Mh Mtawa.

Akizungumza kwenye kikao na madiwani mkuu wa mkoa wa Njombe Dokta Rehema Nchimbi amesema kuwa kata ya Mh MTAWA imefanya vizuri kwenye zoezi la kaya kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF hivyo atatoa zawadi ya pikipiki kwa diwani huyo wa Tandala ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete.

Kwa upande wake  mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete ambaye pia ni diwani wa kata ya Tandala Mh EGNATIO MTAWA anamshukuru mkuu wa mkoa wa Njombe juu ya tuzo hiyo ya pikipiki ambapo pia amesema kuwa watahakikisha wanufaika wa mradi wa TASAF awamu ya tatu wanaunganishwa na mfuko wa afya ya jamii CHF.




JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo