Wazazi waelezea "Ushirikina" unavyotesa watoto wa kike tu wanaosoma Ikonda Makete (Audio)

Hatimaye hali ya kuanguka wanafunzi mara kwa mara katika shule ya msingi Ikonda iliyopo katika kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe imejirudia tena tangu iripotiwe mwaka jana na kutulia kwa muda hali iliyoilazimu kamati ya shule kuitisha mkutano na wazazi ili kuangalia namna ya kulimaliza tatizo hilo.

Akizungumza katika mkutano huo Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ikonda Bw.Keneth Mgana amesema hali hiyo imeanza tangu mwakajana mwezi Aprili na baada kukaa na wananchi lilitulia na limejirudia tena vile vile mwezi wa tatu mwaka huu na watoto wanaokumbwa na tatizo hilo ni jinsi ya kike pekee ambapo hadi sasa wamefikia 6.

Aidha ameongeza kuwa tatizo hilo limekuwa likiathiri kiwango cha taaluma shuleni hapo kwani linapojitokeza tatizo la mtoto kuanguka vipindi vyote husimama.

Kwa upande wao baadhi ya wazazi waliohudhuria mkutano huo wameonesha kusikitishwa na vitendo hivyo na kuwaomba viongozi wa dini na jamii kwa ujumla kuliweka suala hilo katika maombi ili kulimaliza tatizo hilo shuleni hapo.

Nao wazazi wa watoto wanaoanguka mara kwa mara wakatoa ushuhuda hali inayowakumba wakati wa kuwahudumia watoto wao.

Naye afisa mtendaji wa kijiji cha Ikonda Raphael Tweve amewataka wananchi wa kata ya Tandala kujiridhisha na taarifa za wageni wanaoingia katika kata ya Tandala na kuacha tabia ya kuuza viwanja kwa watu ambao hawana taarifa zao kuhusu maeneo walikotoka.

Na Fadhili Lunati


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo