Taharuki imetanda nchini Uganda
baada ya kiongozi wa upinzani Dr Kizza Besigye, ''kujiapishwa kama
rais'' siku moja tu kabla ya kuapishwa rasmi kwa rais Yoweri Museveni .
Haijulikani
ni vipi Dr Kiiza Besigye alikwepa kizuizi cha polisi na kuibukia mjini
Kampala ambapo alikutana na wandani wa chama chake na ''kula kiapo cha
urais wa taifa hilo''.
Katika video inayosambaa kwenye mitandao ya
kijamii Dr Besigye anaonekana ''akila kiapo'' mbele ya mtu aliyevalia
mavazi sawa na ya ''jaji wa mahakama ya juu''.
Video hiyo
imesambazwa mno kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha mamlaka
inayosimamia mawasiliano nchini Uganda kuamrisha kampuni zinazotoa
huduma za simu nchini humo kufunga huduma za mitandao ya kijamii
Besigye anahitimisha 'kuapishwa kwake'' kwa kuonya kuwa ''endapo
kutafanyika sherehe nyengine hapo kesho, basi itakuwa ni kinyume cha
sheria kwani kulingana naye Museveni hakushinda uchaguzi wowote''.
Mgombea
huyo wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Forum for
democratic change FDC- alikamatwa na polisi kwa'' kukaidi amri halali''.
Matukio
hayo yanawadia wakati ambao viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki na
wageni mashuhuri wameanza kuwasili mjini Kampala ilikuhudhuria kuapishwa
kwa rais Museveni hapo kesho.
Tangu matokeo ya uchaguzi
kutangazwa mwezi Februari, Dr Kiiza Besigye amekuwa chini ya ulinzi
mkali nyumbani kwake baada ya kupinga matokeo yaliyompa rais Museveni
ushindi.
video hii hapa
