Na Fadhili Lunati, MAKETE
Wananchi waliopokea msaada wa chakula katika kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kutumia vizuri chakula hicho kwa malengo yaliyokusudiwa na si kutumia kukorogea pombe ili kiweze kuwasaidia katika mahitaji yao ya kila siku.
Rai hiyo imetolewa leo na mwenyekiti wa kijiji cha Tandala Bw.Andowise Memba alipokuwa akizungumza na kituo hiki wakati wa ugawaji wa chakula hicho zoezi lililofanyika hii leo katika ofisi ya kijiji cha Tandala.
Andowise amesema kuwa zoezi hilo limewalenga wananchi wanaoishi katika mazingira magumu ambao wapo katika mpango wa kunusuru kaya maskini(TASAF).

Aidha amesema msaada huo wa chakula ni mahindi na umelenga vijiji vitatu vya kata ya Tandala ambavyo ni Tandala,Ihela na Usagatikwa.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopokea msaada huo wameishukuru serikali kwa msaada huo na kuahidi kuyatumia kwa malengo yaliyokusudiwa.