Zoezi la kuua Mbwa Tandala Makete, Wananchi wachachamaa (Audio)

Kutokana na mbwa wengi kuzagaa mtaani na kusababisha uhalibifu mkubwa kama kula kuku,mayai,mbuzi,na baadhi ya watu kung’atwa na mbwa hao, wito umetolewa kwa wamiliki wote wa mbwa  kuhakikisha wanafungia mbwa hao bandani vinginevyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.   
Hayo yamesemwa na wakazi wa kijiji cha Tandala kata ya Tandala Wilayani Makete mkoani Njombe katika mkutano uliofanyika kijijini hapo ambapo kila mwananchi anatakiwa kuwa mlizi kwa kuhakikisha mbwa yeyote atakayeonekana kuzurura mtaani lazima auwawe bila kujali mbwa huyo ni wa nani.                  
Hata hivyo wananchi hao wame kubaliana kuhakikisha watakuwa bega kwa bega kuhakikisha mbwa wote walio kuwa wa kizurura ovyo mtaani wana tokomezwa kwani wamekuwakero kubwa kijijini hapo.

Utekelezaji wa zoezi hilo la kuua mbwa wanaozurura limenza mala moja hapo jana mara baada ya wananchi kukubaliana huku mwenyekiti wa kijiji hicho Andowisye Memba na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bw, Ambele Sanga wakiwaomba wananchi kuanza utekelezaji.

Na Asukile Mwalwembe


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo