Na Daudi Manongi- MAELEZO
HALMASHAURI
za Miji na Wilaya nchini zimekumbushwa kukamilisha zoezi la upatikanaji
wa madawati kwa shule za msingi na sekondari ifikapo juni 30 mwaka huu
ili kutekeleza agizo lililotolewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini
katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Rebecca Kwandu wakati wa mahojiano na mwandishi wa habari hizi kuhusu
uchakavu wa madarasa na ukosefu wa madawati unaozikabili shule za kinesi
A na B zilizopo wilaya ya Rorya mkoani Mara.
“Suala
la upungufu wa madawati na uchakavu wa madarasa ni changamoto ya
kitaifa na kwamba lilishatolewa agizo na mheshimiwa Rais John Pombe
Magufuli kuhusu halmashauri zote nchini kuhakikisha ifikapo Juni 30
mwaka huu kila mwanafunzi anaketi kwenye Dawati” Alisema Kwandu.
Kwa
mujibu wa Gwandu alisema Serikali ya awamu ya tano imepania kuinua
kiwango na ubora wa elimu nchini kupitia mikakati na sera ya elimu bure
nchini kote.
Aliongeza
kuwa hatua hiyo imeibua changamoto kubwa kwa wanafunzi wengi kujitokeza
kwa asilimia kubwa na hivyo ni wajibu wa halmshauri hizo kukidhi
mahitaji ya madawati ili wasome katika mazingira mazuri.
“Mpaka
sasa Serikali imeendelea kutoa pesa kwa ajili ya elimu bure nchini kote
na kumekuwepo kwa changamoto mbalimbali kama upungufu wa
walimu,madawati na madarasa ambapo serikali inafanya jitihada za kila
namna ili kutatua changamoto hiyo”
Akifafanua
zaidi Gwandu alisema Serikali inaandaa harambee mbalimbali na kuongeza
wigo wa utoaji wa vibali vya kuchangia maendeleo ya elimu kwa hiari ili
kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali wenye nia ya kufanya.