Wananchi wa Tandala Makete wachachamaa, Wavamia kituo cha Polisi, (Picha na Audio)

Kutokana na kuendelea kushamiri kwa matukio ya wizi katika kijiji cha Tandala kata ya Tandala wilayani Makete mkoani Njombe, wananchi wameombwa kuwa watulivu na kutojichukulia sheria mikononi huku jeshi la polisi likitahadharishwa kuwachukulia sheria ipasavyo watuhumiwa wanaofikishwa kituoni na wananchi

Hayo yamesemwa hii leo katika kituo cha polisi Tandala na Diwani wa Kata ya Tandala Mh. Egnatio Mtawa Baada ya wananchi kuwakamata watuhumiwa wa wizi ambao mpaka tunakwenda mitamboni majina yao hayajapatikana vizuri, na kuwafikisha kituoni hapo na wananchi kuonesha kukerwa na vitendo hivyo

Aidha baada ya watuhumiwa hao kufikishwa kituoni hapo wananchi walikizingira kituo hicho wakishinikiza watuhumiwa hao kuchukuliwa hatua na ndipo diwani huyo akazungumza na wananchi waliofika kituoni hapo pamoja na askari waliokuwepo kituoni hapo wakiongozwa na mkuu wa kituo, kuwa wananchi wanahitaji kujua hatma ya tukio hilo na mtandao mzima wa wizi ulioanza kushamiri katika kijiji hicho



Baadhi ya wananchi wakazungumzia tukio hilo na kutoa maoni yao na kusema inauma kuona watuhumiwa wengine kuhukumiwa kifungo kidogo ukilinganisha na kosa walilofanya

"Unakuta mfano umeibiwa pikipiki ya milioni moja na nusu mtuhumiwa anafungwa miezi 8 jamani hili linatuumiza wananchi" alisikika mwananchi mmoja ambaye hakutaja jina lake



Mkuu wa kituo cha polisi Tandala Afande Majiruka akatoa rai kwa wananchi kuwaomba wanapowakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye kituo cha polisi wasijichukulie sheria mikononi kwa kuwapiga kwa lengo la kuwaua kwa kuwa ni kinyume cha sheria

Hadi sasa jeshi hilo la polisi linawashikilia watuhumiwa hao wanne kwa hatua zaidi za kisheria huku wananchi wakisubiri kufahamishwa ni nini kinaendelea katika kesi hiyo

 Msako ukiendelea kusaka mali za wizi kwa watuhumiwa
 Watuhumiwa wa wizi wakijitetea

 Watuhumiwa wa wizi wakiwa wamefungwa pingu wakaoneshe walikoficha mali za wizi

 Utafutaji mali za wizi ukiendelea

 Ni msako katika kila walipokuwa wakitaja

 Watuhumiwa wakipelekwa kituo cha polisi Tandala

 Wananchi wakiwa kituo  cha polisi Tandala kujionea tukio hilo

 Diwani wa kata ya Tandala akizungumza na wananchi waliofika kituoni hapo akiwaomba waondoke



JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo