Mh Egnatio Mtawa
Hayo yamesemwa na mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha sita katika shule hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa yaliyofanyika Ijumaa April 22 ambapo pamoja na mambo mengine amewasisitiza wanafunzi hao kufanya vizuri katika mitihani yao inayokuja na kuwa na moyo wa kusoma zaidi na zaidi ili wafike mbali kielimu
Pia ametoa wito kwa wananchi wa tarafa ya magoma kujitolea kukarabati BWENI LA shule hiyo kwa kuwa ni mali yao na shule hiyo inaendelea kuelimisha jamii bila ubaguzi wala upendeleo kama serikali inavyotaka
katika risala ya wahitimu hao iliyosomwa na Isaya Michael imetaja baadhi ya changamoto zinazoikabili shule hiyo kuwa ni pamoja na uchakavu wa mabweni hasa ya wasichana, ukosefu wa bwalo pamoja na uchache wa nyumba za waalimu
Mwalimu akihojiwa na Mwandishi Dj Nundu
Mkuu wa shule Mwakavuta
Wanafunzi wahitimu wakiwa na Mkuu wa PCCB Makete
Mwalimu nae akipokea zawadi
Mhitimu akipokea cheti
wahitimu wa kidato cha sita
wanafunzi waagwa