Wanafunzi watupiwa uchawi na Wazazi wao huko Mtwara

Tuhuma za ushirikina zimeibuka katika kijiji Mnyawa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba katika mkoa wa Mtwara ambapo wakazi wake wanadaiwa kufanya vitendo hivyo dhidi ya wanafunzi ikiwa ni sehemu ya wao kupinga wasifanye vizuri kwenye masomo yao

madai hayo yametolewa na mwalimu mkuu wa shule ya Mnyawa Makeeja Maduhu baada ya tukio la hivi karibuni la wanafunzi zaidi ya 14 kukumbwa na ugonjwa wa ajabu wa kuanguka na kupoteza fahamu

Mashuhuda wa tukio hilo wanasema wanafunzi hao walianza kuanguka majira ya saa moja wakati wakifanya usafi shuleni hapo


Mkuu wa wilaya hiyo Emmanuel Wahula amekemea vitendo vya wananchi hao kukwamisha maendeleo ya elimu wilayani hapo


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo