Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza waziri wa Kilimo na Mifugo Mwiguli Nchemba kuwanyang’anya vitalu vya ufugaji wawekezaji walivyomilikishwa na kampuni ya ranchi ya taifa kwa ajili ya ufugaji wa kisasa na wa kibiashara ambao wanavitumia kinyume.na malengo ili wagawiwe wananchi.
Waziri mkuu huyo amesema wanaotakiwa kunyang’anywa vitalu walivyomilikishwa ni pamoja na wale walioshindwa kuviendeleza na wanaokodisha maeneo ya vitalu hivyo kwa wageni toka nje nchi wanaoingia hapa nchini na mifugo yao,amesema wageni ndio chanzo cha migogoro kati ya wawekezaji na wananchi, pia amepiga marufuku viongozi wa seriali ngazi za vijiji na kata kutoa vibali kwa wageni toka nje ya nchi kwa kuwa vibali hivyo ndivyo vinawapa uhalali wa kuingiza mifugo yao.
Kwa upande wake,waziri wa kilimo na mifugo Mwigulu Nchemba ameeleza kuwa serikali kamwe haitamuonea mtu wakati wa zoezi la kuwabaini wanaotumia vitalu kinyume na malengo,amesema zoezi hilo litafanyika kwa umakini mkubwa na halitawasalimisha wanatumia vitalu hivyo kufanya shughuli ambazo niu haramau ambazo ni pamoja na ulimaji wa bangi ukataji miti kwa ajili ya uchomaji wa mkaa.