Idara ya uhamiaji mkoani Geita inawashikilia raia 13 wa China kwa tuhuma
za kufanya kazi za kutafiti pamoja na kufanya kazi za kuchenjua madini
ya dhahabu kinyume cha sheria.
Watuhumiwa
hao wamekamatwa katika machimbo ya Igo katika kijiji cha Nyamahuna
wilayani Geita kufuatia msako mkali kwa wageni wa mataifa kutoka nje
wanaofanya kazi mkoani humo bila ya kuwa na kibali.
Akizungumza mara baada ya kuwakamata watuhumiwa hao afisa uhamiaji
mkoa huo Charles Washima amesema watuhumiwa hao waliingia nchini kwa
kibali cha matembezi lakini wamekuwa wakijihusisha na ufanyaji kazi
kinyume na sheria.
Naye mmiliki wa mgodi huo Bi. Rehema Abdallah alishikiliwa na Idara
hiyo baada ya kuhusika na kuwaleta raia hao wachina kufanya kazi katika
mgodi wake bila ya kuwa na kibali maalum