Msanii
huyo amefunguka na kusema hajutii kabisa alichokifanya kwenye wimbo ule
kwani yeye anaamini alichokifanya ni kitu sahihi na ukweli.
"Nashukuru kwa support kubwa niliyopata kwa mashabiki kwani tangia
nimeanza muziki haijawahi kutokea nimepata support kama kwenye wimbo
huu, lakini niseme ukweli ni kwamba sijutii kabisa mimi kufanya kazi hii
kwani mimi naamini kuwa nilichokifanya ni kitu sahihi kwani
nimezungumza ukweli ambao upo" Alisema Nay wa Mitego.
Mbali na hilo msanii huyo amesema kuwa kwa sasa kuna watu ambao
wamekuwa wakimfuatilia kwa njia ambayo yeye mwenyewe haelewi nia yao, na
kusema kuwa juzi kuna gari ilikuwa ikimfuatilia lakini aliweza
kuichenga.
Amesema hata hivyo hajutii kufanya wimbo huo na amedai siku za
mbeleni atafunguka mengi zaidi ambayo yanamtokea sasa kutokana na ngoma
hiyo.
Pia mkali huyo kupitia ukurasa wake wa Instgram ameweka bayana kuwa
atatoa video ya wimbo huo 'Shika adabu yako' ambao kwa sasa umefungiwa
na BASATA.
"Ahsanteni watu wangu wa Kusini 'Shika adabu yako' hii ngoma nadhani
kwangu haijawai tokea. Sitaki kuamini kuwa mpaka huku mikoani tayari ni
wimbo unaoimbwa na kila mtu kama imetoka miezi miwili iliyotoka.!!
Faraja niliyonayo haielezeki.Next week au this week Video itakua Kwenye
Tv yako na YouTube na mitandao yote. Kaa tayari wewe" Alimalizia Nay wa
Mitego.