Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ndiyo yenye
dhamana ya kusimamia huduma za afya kwa wananchi imesema itaendelea
kutoa taarifa za mara kwa mara kwa wananchi kuhusu milipuko ya magonjwa
ikiwamo kipindupindu.
Taarifa
hiyo iliyotolewa kwa vyombo vya habari imewataka viongozi wa mikoa na
wilaya kuhakikisha upatikanaji wa taarifa sahihi, mapema kwa kuzingatia
miongozo na kwa wakati bila kuficha pindi wanapopata wagonjwa wapya.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa jamii isiwekewe vikwazo vya faini au kunyanyapaliwa wapatapo ugonjwa huo kwani inaweza kusababisha wananchi kuogopa kwenda katika vituo vya afya.
Aidha imewataka wakuu wa mikoa na wilaya wawasiliane na wizara iwapo kuna ufafanuzi wowote unaohitajika kwa taarifa zinazotolewa kuhusu magonjwa hayo ya mlipuko.