NA VICTOR MASANGU, PWANI
WANANCHI zaidi ya 5000 katika
Wilaya ya rufiki Mkaoani Pwani kwa sasa hawana mahali pakuishi kutokana
na nyumba zao kukumbwa na mafuriko kutokana na mvua kubwa zinazoendelea
kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini.
Kufuatia kutokea kwa mafuriko
hayo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injiania Evarist Ndikilo amekwenda katika
eneo la tukio na kujionea athari zilizojitokeza kwa wananachi hao wa
wilyani rufiji kutokana na mvua hizo zilizosaababisha mafuriko.
Akizungumza na wahanga wa
mafuriko hayo Ndikio alisema kwamba kutokana na hai hiyo serikali Mkoa
wa Pwani imechukua hatua za haraka kuwasaidia wananci hao kwa kutoa
chakula cha dharura tani 1283 za mahindi kwa ajili ya wananchi hao.
Ndikilo alisema kuwa mbali na
serikali kutoa tani hizo za mahindi pia imetoa mbegu za mahindi tani 10
sambamba na tani 5 za mtama ambazo zinastawi kwa kipindi cha mudamfupi
ii wannaachi waweze kuzipanda katika ukanda wa juu ii ziweze kuwasaidia
katika upatikanaji wa chakula.
“Kwanza kabisa mimi nawapa pole
wale wote ambao wamepata na maafa haya ya mafuriko na wengine kukosa
sehemu ya kuishi lakini nataka kuwahakikishia kuwa serikali yenu ipo
pamoja nanyi katika kuhakikisha unawasaidia huduma zote muhimu ambazo
zinastaili ikiwemo kuwapatia chakula kw ahiyo msiwe na hofu yoyote,”
“Lkini ombi langu kubwa kwa
kipindi hiki kwa wanaanchi ni kuwa makini sana kwani mvua bado
zinaendelea kunyesha na na zimeleta maafa makubwa kama mnavyoona kwa
hiyo cha msingi kama kuwa wnanchi bado wanaendelea na shughuli za kulima
karibu na mabonde ya mito wasiendelee kulima katika maeneo hayo kwani
wanaweza kusombwa na maji,”alifafanua Ndikilo.
Pia Ndikio aliwaomba wahanga
hao wa mafuriko kuhakikisha wanakitumia vizuri chakula amabcho
kimetolewa na serikali kwani katika kipindi hiki uende mahitaji ya
chakula yakaongezeka zaidi kutokana na mahitaji mwengi ya wananchi
wenywe hivyo ni vema kuwa na matumizi mazuri.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa alisema kwa sasa kazi kubwa inayofanywa na serikali ni kutoa elimu kwa wananachi na kuwahamasisha wale wote waliokumbwa na mafuriko watoke mara moja katika maeneo ya mashamba kwani ni hatari kwa masiha yao pindi mvua inaponyesha.
Akizungumzia kuhusina na baadhi ya wafanyabiashara amabo
wamekuwa na tabia ya kupandisha bei ya vyakula pindi wnapoona maafa kama
hayo yamejitokeza waacha mara moja kufanya hivyo kwani ni kwakandamiza
wananchi.
” Wafanyabiashara
wasiowaungwana wasitumie janga hili kujinufaisha kwa kupandisha bei ya
vyakula, kwa kutambua hilo tumewapa vibali wafanyabishara 6 wenye uwezo
ili wanunue tan 10 za mahindi na kusaga unga na kuwauzia wananchi kwa
bei nafuu kwa jimbo la kibiti na ikwiriri,” alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Rufiji Nurdin Babu aibainisha kuwa kutoka ana mvua hizo zinazoendelea kunyesha tayari jumla ya hekta 8138.4 za mpunga na tani 7171.2 za mahindi zimeathirika na maji na kuwa mazao hayo yalikuwa katika hatua za mwisho kwa ajii ya kuvunwa.
Babu aliongeza mafuriko
yaliyotokea katika wilaya yake yalianza tangu juzi usiku na kuvikumba
vijiji mbali mbali ikiwemo kijiji cha uwe na mhoro na kusababisha
daraja la muhoro kuvunjika na hivyo wananchi kuvuka kwa kutumia mitumbwi
pamoja na boti.
