Nape: Nikisema Ukweli naonekana Mkorofi

Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi kupitia tiketi ya CCM, Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa ya moyoni kwa kusema kila anapokumbuka shida wanazozipata wananchi humfanya aonekane mkorofi kwa kuwa anasema ukweli.

Nape amebainisha hayo, kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter huku akiwa ameambatanisha na picha ambayo inaonesha wananchi jinsi wanavyopata tabu kuvuka upande mmoja wa mto kwenda upande wa pili kwa kupita ndani ya maji hayo.

“Niliyashuhudia maisha haya mikoani kwa miezi 38, nadhani ndiyo nikiyakumbuka naonekana mkorofi !! iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu”. Ameandika Nape

Niliyashuhudia maisha haya mikoani(38months),nadhani ndio nikiyakumbuka naonekana mkorofi!!Iko haja kama Taifa kuangalia vipaumbele vyetu!


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo