Polepole: CHADEMA imekata Kauli, bado Kidogo Ife Tuizike

KATIBU wa itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole amesema kwa sasa chama cha demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kimekata kauli hivyo muda wowote kuanzia sasa kitafanyiwa maziko

Polepole ameyasema hayo hivi karibuni katika mji wa Tunduma mkoani Songwe mara baada ya kuwapokea viongozi wa CHADEMA Wakiwemo madiwani na wanachama zaidi ya 600 walioamua kujiunga na chama hicho na kusema wameamua kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kazi nzuri anazoendelea kuzifanya hapa nchini

Amesema kwa sasa CHADEMA imefikia kikomo chake kwa sababu chama hicho kimeshakata kauli hivyo yeyote anayefahamu anajua mtu akishakata kauli kinachofuata ni kifo na hatimaye maziko


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo