Kande zamaliza utoro wa wanafunzi shule ya Msingi Ludihani Makete

Utoro katika shule ya Msingi Ludihani wilayani Makete mkoani Njombe umepungua kwa kiasi kikubwa baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuanza kupatiwa chakula cha mchana shuleni hapo tangu Januari 25 mwaka huu

Katika kikao cha wazazi kilichofanyika shuleni hapo mwezi uliopita kwa kauli moja waliazimia ifikapo Januari 25 mwaka huu wanafunzi waanze kula chakula cha mchana ambacho ni kande jambo ambalo limetekelezeka baada ya wazazi na walezi kuchanga fedha za chakula

Akizungumza nasi mwalimu mkuu wa shule ya Msingi Ludihani Onesmo Chang'a amesema kwa sasa utoro shuleni mwake umepungua huku wanafunzi wakifurahia kuanza kula shuleni na wengi wao wakihudhuria vipindi hasa vya mchana ambavyo mahudhurio yalikuwa mabaya hasa baada ya kwenda nyumbani kwa ajili ya kula chakula

"Kwa sasa wanafunzi wanakula shuleni kila siku za shule isipokuwa Jumatano ambayo wanafunzi hutoka mapema kwa ajili ya kwenda kufanya usafi hasa wa sare zao za shule, wazazi wengi wa hapa Ludihani wanathamini sana Pombe kuliko kuwapatia watoto chakula, sia ajabu ukakuta watoto wakila kande za shule wakifika nyumbani hawakuti chakula" amesema Chang'a

Hapo awali wanafunzi hao walikuwa wakinywa uji tu shuleni hapo jambo ambalo halikuonesha mafanikio kwa wanafunzi hao hadi mwanzoni mwa mwaka huu wazazi kupitia kikao chao walipokubaliana kwa pamoja kuchanga fedha ili wanafunzi hao waanze kupata chakula shuleni


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo