Hali ya ugonjwa wa Saratani hapa nchini ni Mbaya

Februari, 4 ya kila mwaka huwa kunafanyika maadhimisho ya siku ya Saratani duniani ambapo kwa nchini Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto imetoa taarifa ya hali ya ugonjwa huo ilivyo nchini.
ps2ps2Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili kufanyiwa vipimo bure vya Saratani ya tezi dume, shingo ya kizazi na saratani ya matiti.
Akizungumza na waandishi wa habari. Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Mpoki Ulisubisya alisema hali nchini sio nzuri na kuwa wagonjwa wa ugonjwa huo wamekuwa wakiongezeka kila mwaka na wengi wao wamekuwa wakifika hospitalini wakiwa tayari ugonjwa wao upo katika hali mbaya.
Alisema Tanzania ina wastani wa wagonjwa 44,000 kila mwaka na 4,400 hufariki kwa sababu ya saratani kuwa imefikiwa hatua ambayo ni ngumu kumuokoa mgnjwa na hiyo ni idadi ya wanaofika hospitalini lakini wanaamini bado kuna wengine hawafiki kupata tiba.
“Tatizo la Saratani limekuwa likiongezeka na kukua, kila mwaka takribani wagonjwa wapya wapatao 44,000 hugundulika na saratani za aina mbalimbali nchini, hii ni sawa asilimia 10 tu (4,400) kati ya wagonjwa wote wanaofanikiwa kufika katika Taasisi ya Saratani Ocean Road ili kuweza kupata tiba,” alisema Ulisubisya.
Aidha alitaja mambo yanayopelekea mtu kupata ugonjwa huo kuwa ni pamoja na ulaji usiofaa mafuta na sukari, uzito uliozidi, unene uliokithiri, kutofanya mazoezi, uvutaji wa sigara na bidhaa zitokanazo na tumbaku, na unywaji pombe kupita kiasi.
ps3ps3Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya kuhusu siku ya maadhimisho ya Saratani duniani inayotarajiwa kufanyika Februari 4.
Katibu Mkuu huyo aliwataka wananchi kuweka utaratibu wa kwenda katika vituo vya afya kwa ajili ya kujua afya zao kwani ugonjwa huo umekuwa si rahisi kuonyesha dalili za awali na wengi huwa wanajua kama wanaumwa baada ya ugonjwa kufikia katika hatua mbaya.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dkt. Julius Mwaiselage alisema kuwa kuelekea kwenye siku hiyo ya ugonjwa wa saratai, taasisi yao itatoa huduma ya upimaji bure wa vipimo vya saratani ya tezi dume, saratani ya shingo la uzazi na saratani ya matiti.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo