Alichokifanya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa hii leo

Waziri Mkuu Majaliwa Kasim Majaliwa mapema leo amezindua mkutano wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi  wenye lengo la kusaidia wananchi na maendeleo katika Nyanja mbalimbali zikiwemo kuanzia ngazi ya kijiji, Kata, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Mkutano huo ulioandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)  unaondelea katika ukumbi wa Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,  unawakutanisha wadau kutoka sekta mbalimbali  ikiwemo za Serikali na zile za binafsi pamoja na wadau mmoja mmoja katika kuleta fursa za kimaendeleo na kunufaika kwa uchumi.

Wakati wa uzinduzi huo, Waziri Majaliwa ameeleza kuwa, watu binafsi wananafasi ya kipekee katika kusukuma mbele kurudumu la kiuchumi ikiwa tu wataendelea kushirikiana na Serikali hasa katika mipango yao ya kimaendeleo.

“Wadau mbalimmbali muliopo hapa nan je. Chachu ya ukuaji wa kiuchumi kwa wananchi wetu ni kwa kushirikiana na nyie. Hivyo tunawakaribisha sana na pia musisite mara kwa mara kufika katika ofisi zetu hasa za Wakuu wa Mikoa ili name niletewe taarifa..maana moja ya majukumu yangu ni kuongea na wananchi likiemo ili la ukuaji wa kiuchumi kwa wananchi wetu” amebainisha Waziri Mkuu katika ufunguzi huo.

Imendaliwa na Andrew Chale,modewjiblog
majaliwWaziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
maliwae Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akiwa ameshikilia kitabu chenye muongozo wa mpango kazi wa uwezeshaji wananchi. wengine ni viongozi wa Serikali na wadau kwenye ufunguzi huo wa  Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
majliwa4Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi nakala yenye muongozo na fursa za kiuwezeshaji uchumi kwa wananchi, Mwenyekiti wa bodi ya Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) Dkt. Reginald Mengi  wakati wa Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji  Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9, 2016. (Picha na Andrew Chale,modewjiblog).
majaliwa6Baadhi ya wadau kwenye mkutano huo wakiwemo viongozi wa Serikali na wale kutoka taasisi binafsi.(Picha na Andrew Chale).
majaliwamodewjiblog2Moja ya mabanda ya maonyesho yaliyopo kwenye mkutano huo. Pichani ni baadhi ya maafisa wa PSPF wakiendelea kutoa huduma kwa wananchi iwanaotembelea katika banda hilo (Picha na Andrew Chale).
maliwadd Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia  au Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu).
majaliwakasim
majaliwa90
majaliwa modewjiblog
Baadhi ya washiriki wa TIB
DSC_2914Baadhi ya washiriki kutoka UTT MicroFinance
majaliwa548Waziri Mkuu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa serikali, sekta binafsi pamoja na wadau wengine katika mkutano huo unaoendelea jijini Dar es Salaam. (Picha na Andrew Chale)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo