Kuhusu Askofu Gwajima kuzushiwa kifo

Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, jana alizushiwa kuwa amefariki dunia.

Taarifa hizo zilizozagaa katika mitandao ya kijamii zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia katika hospitali ya TMJ, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa hizo zilienea  kuanzia ya saa tano asubuhi, zilieleza kuwa Askofu Gwajima alifariki dunia kwa shinikizo la damu. 
 
Hata hiyo, taarifa hizo zilikanushwa vikali na mwanasheria wake, wakili wa kujitegemea Peter Kibatala.

Kibatala jana alisema taarifa hizo ni za uzushi ambao haelewi chanzo chake.

“Nimesikitishwa na taarifa hizi na nimepigiwa simu nyingi sana leo kuniuliza juu ya kifo cha Askofu Gwajima na nimebaki nashangaa kwani ni mzima wa afya,” alisema Kibata.

Majira ya jioni jana picha zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii ziliomwonyesha Askofu Gwajima akiwa mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo