Treni ya jiji yapata ajali


Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Januari 22, 2016. 

Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mabehewa yake matano ya treni hiyo kupata ajali ya kuacha njia mara baada ya kuondoka kituo cha Kamata.wakati wa huduma ya asubuhi ikitokea Ubungo Maziwa.

Kwa sasa mabehewa hayo yanafanyiwa ukaguzi ili yaweze kurekebishwa kasoro ndogondogo tayari kwa kuendelea na huduma siku ya Jumatatu ijayo. Januari 25, 2016. Huduma ya treni ya jiji hutolewa kwa siku 5 kwa wiki ambapo ni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, isipokuwa kwa siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu za Kitaifa.

Atakayesoma taarifa hii amuarifu mwenziye.



Uongozi wa TRL unasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza.

Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa Niaba ya :
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL,
Mhandisi Elias Mshana,
Dar es Salaam,
Januari 22, 2016


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo