Jecha azinduka....atangaza siku ya kurudia uchaguzi wa Zanzibar

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imetangaza tarehe ya marudio ya uchaguzi visiwani humo baada ya matokeo ya uchaguzi uliopita kufutwa.

Uchaguzi huo sasa utafanyika Jumapili tarehe 20 Machi 2016.
Tangazo hilo limetolewa  na mwenyekiti wa ZEC Jecha Salim Jecha.

Jecha amesema tarehe hiyo iliamuliwa na tume baada ya mkutano hapo jana.

"Uchaguzi huo utahusisha uchaguzi wa Rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani na hakutakuwa na uteuzi mpya wa wagombea wala mikutano ya kampeni," amesema Bw Jecha.



"Wagombea wote walioteuliwa hapo awali wataendelea kuwa wagombea katika uchaguzi huu."


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo