Na Saimeni mgalula,Momba
WANANCHI wa JImbo La Tunduma lililopo Wilayani Momba Mkoani Mbeya ,wametakiwa kutokulima au kupanda mazao ya aina yoyote katika makazi yao wanayo ishi  kutokana na jimbo hilo kuwa Mji wa halmashauri ya Tunduma hivyo haitakiwi kisheria .
Rai hiyo ilitolewa na  Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Tunduma vile vile ni Diwani wa kata ya Makambini  Jana alipokuwa akizungumza nasi Ally Mwafongo kupitia chadema alisema endapo mtu atakiuka agizo hilo la serikali atachukuliwa hatua za kisheria.
Mwafongo alisema kutokana na baadhi ya wakazi walikuwa na mashamba sehemu za katikati ya mji na wamelima hivyo tutawaacha wavune mzao ya kwa mwaka huu na mwakani haitatakiwa kulima tena tumewapa ofa hiyo ni kutokana na wao kuwa na maeneo makubwa .
‘’Tumeamua kuwapa ofa kutokana na kuchelewa kuwapa taarifa mapema na wao walikuwa hawajui kuwa ukisha kuwa mji hautakiwi kulima wala kupanda mazao ya aina yoyote’’alisema
Mwenyekiti huyo alisema maeneo hayo inatakiwa yapimwe kama viwanja vingine na kama hawataki kuvipima viwanja hivyo basi wavitumie kwa shughuli zingine lakini sio kwa kulima hasa zao la mahindi ambalo wakazi wengi wamepanda kwenye kaya,alisema Mwafongo
Alisema suala hili limeongelewa ni zaidi ya mwezi sasa hivyo oparesheni itapita mitaani kwao huko huko kwa kushirikiana na watendaji wa kata  na wa serikali za maitaa kuakikisha kuwa wananchi wanakuwa chini ya sheria,alisema,
‘’Kutokana na serikali kutoa kamko hilo na wakazi walishatangaziwa hivyo basi kwa mtu ambaye atakuwa amekiuka sharti atapigwa atachukuliwa hatua kali za kisheria za kutokutii amri ya serikali’’alisema
Aliongeza kuwa watendaji wa serikali za mitaa na wnyeviti wao wapiti katika makazi yao au waitishe nikutano ili wananchi wajue taarifa hizo za kutokulima katika makazi ambayo watu wanaishi haitakiwi,alisema mwafongo.
