Kilichotokea kwenye ziara hii ya kushtukiza wilayani Makete

 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh Egnatio Mtawa (wa pili kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Afisa kutoka Idara ya Mifugo halmashauri ya wilaya ya Makete.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Makete Mh. Egnatio Mtawa amefanya ziara ya kushtukiza katika machinjio ya Mji mdogo wa Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe na kujionea utendaji kazi ambapo imemlazimu kutoa maagizo

Ameshuhudia jinsi wanavyochinja mifugo katika machinjio hiyo pamoja na kupokea kero mbalimbali kutoka kwa mwenyekiti wa wachinjaji Bw. Abraham Mbilinyi kwa kumweleza kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme, eneo la machinjio kuingiliwa na makazi ya watu, kukosekana kwa uzio pamoja na kuletewa ankara kubwa ya maji ambayo inatilia mashaka

Kufuatia changamoto hizo mwenyekiti huyo ameonesha kutoridhishwa na hali ya usafi katika machinjio hiyo kwa kuagiza hali ya usafi iongezeke hasa kipindi hiki kukiwa na mlipuko wa magonjwa mbalimbali pamoja na kutoa siku saba mfereji unaochuja takataka kabla hazijasafiri kwenda shimo maalum la kuzitupa urekebishwe kwa kuwa mambo yanafanywa kienyeji

Baada ya ziara hiyo pia amefanya ziara nyingine kwenye vizimba vya kutupa takataka vilivyopo Makete mjini, ambapo pamoja na mambo mengine ameagiza kuongezwa muda wa kuzolewa takataka katika vizimba hivyo, kutokana na halmashauri kutoza fedha za kusomba takataka kutoka kwa watu hivyo zinavyokaa muda mrefu bila kusombwa inapelekea wananchi kutoielewa halmashauri yake

 Machinjio hiyo kwa ndani
 Mwenyekiti wa halmashauri ya Makete Mh Egnatio Mtawa akikagua sehemu wanapowekwa ng'ombe muda mchache kabla ya kwenda kuchinjwa

 Shimo la kutupia takataka
 Ziara imemalizika sasa wanaondoka
 Kizimba cha kutupia takataka enao la kona Makete mjini
 Mwenyekiti wa halmashauri akiwa na maafisa mbalimbali wa halmashauri ay wilaya ya Makete wakiendelea na ukaguzi
 Kizimba cha Kutupia takataka eneo la sokoni Makete mjini
 Mwenyekiti wa soko la Makete mjini akitoa utaratibu wa ukusanyaji wa takataka katika soko hilo
Mwananchi akitupa takataka


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo