Polisi mkoani Arusha imebadilisha utaratibu wa kuwaadhibu madereva wa daladala wanaodaiwa kuwa sugu wa kuvunja sheria kwa kuwakamata na kuwaweka ndani badala ya kuwatoza faini urataibu ambao licha ya kuonyesha mwelekeo wa mafanikio umelalamikiwa kwa kiasi kikubwa na wamiliki wa vyombo hivyo vya usafiri
Wamiliki wa vyombo hivyo wamefikisha malamiko yao kwa mkuu wa mkoa wa Arusha kupitia kwa kiongozi wa chama kinachosimamia mabasi madogo ya abiria (daladala) mkoa wa Arusha Bw Adolf Loken licha ya kukiri kuwepo kwa baadhi ya madereva wakorofi amesema wanaendelea kuwadhibiti na amemuomba mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Ntebenda kuingilia kati zoezi hilo kwani lina athari nyingi.
Aidha Bw lokeni amesema utataibu huo wa kuwakamata madereva,kuwafunga pingu na kuwaweka ndani linasababisha madereva kutelekeza abiria na magari yao jambo linalohatarisha usalama wao na magari yao.
Kwa upande wao baadhi ya madereva nao wamelalamikia polisi kwa kuchelewa kuwarudishia leseni zao wanazowanyang'anya wanapopatika na makosa hata baada ya kulipa adhabu ya faini wanazotowa.
Akizungumzia malalamiko hayo mkuu wa mkoa ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa Bw Daud Felexs Ntebenda kijiko amesema adhabu hizo ambazo ziko kisheria zinaztolewa kulingana na mazingira na licha ya kuahidi kufuatilia amesema njia pekee ya kuepukana na matatizo hayo ni kufuata na kuheshimu sheria.
