Mvua zinazoendelea kunyesha Makete mkoani Njombe zimesababisha madhara ya barabara kujifunga eneo la Kisajanilo Iwawa Makete baada ya udongo kuporomoka na kuifunga barabara hiyo itokayo Makete mjini Kwenda Bulongwa
Juhudi za wilaya ya Makete kuwasiliana na Mkoa wa Njombe wakiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo Mh Daud Yassin Zilizaa matunda na kusababisha TANROAD mkoa wa njombe kufika na katapila lililoondoa kifusi hicho na kuifanya barabara hiyo kupitika kama mwanzoni
Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Desemba 9 mwaka huu, angalia picha za tukio hilo
Mkuu wa wilaya ya Makete Daud Yassin (wa kwanza kushoto) akiwa na mhandisi wa ujenzi wilaya ya Makete Bw TEmbo na viongozi wa TANROAD mkoa wa Njombe wakiwa eneo la tukio
Katapila likiwa kazini kuondoa kifusi
Magari yakianza kupita
Mkuu wa wilaya ya makete Daud Yassin akifuatilia kwa ukaribu zoezi hilo hadi lilipokamilika
Baadhi ya abiria waliokwama wakiwa eneo la tukio
Mkuu wa wilaya ya Makete Daud Yassin akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo
Viongozi hao wakiangalia sehemu nyingine inayoonekana kumomonyoka