Dhamira ya dhati iliyowekwa na halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda kwa mwaka 2015 imezaa matunda baada ya ufaulu huo kuongezeka karibia mara dufu
Kwa mujibu wa kaimu Afisaelimu msingi wilaya ya Makete Mwalimu Leopord Mlowe, kiwango cha ufaulu elimu ya msingi kwa mwaka huu kimepanda kwa asilimia zaidi ya 80, jambo lililoonesha kuwa endapo kila mtu akiwajibika kila jambo linawezekana
Hii hapa chini ni kauli yake akielezea sababu zilizopelekea ufaulu kupanda wilaya ya Makete wakati akizungumza na Eddy Blog, bonyeza play kumsikiliza