
Amesema kitendo hicho siyo cha kiungwana na hivyo kulazimika kuwaomba radhi viongozi kutoka zanzibar na kuahidi kitendo hicho hakitajirudia tena.
Amesema wabunge waliomchagua wanaweza kumfanya awe spika mwema na mzuri
Awali wakati wa kuwakaribisha viongozi mbalimbali akiwemo rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh John Magufuli na rais wa Zanzibar mh Dkt Ally Muhamed Shen ndipo viongozi hao wakaanza kupika kelele.
Wakati wa kumkaribisha rais wa zanzibar baadhi ya wabunge waliendelea kupiga kelele na hivyo kumlazimu spika wa bunge kuwataka watoke nje nao wakafanya hivyo.