Mhadhiri huyo ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini amezungumza hayo alipokuwa katika mahojiano maalum na Kituo cha Televisheni cha Azam Two muda mfupi jana baada ya kuapishwa kwa Dk. Magufuli.
Dk. Magufuli ameapishwa leo baada ya kupata ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka huu kwa kupata asilimia 58.46.
Amesema kuwa, Rais Magufuli haanzi kazi mpya bali anaendeleza kazi walizoacha watangulizi wake kuanzia Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere.
Ameeleza kwamba miongoni mwa kazi ngumu zinayomkabili ni pamoja na kumaliza mgogoro kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao unaonekana kutofika mwisho.
Katika mahojiano hao amesema, Rais wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete pamoja na kufanya juhudi zake katika kutatua mgogoro huo, kazi hiyo hakuimaliza.
Ameeleza kwamba hakuna sababu ya kushirikisha mataifa ya nje katika kutatua mzozo wa Zanzibar na kwamba, dukuduku la Muungano linaweza kutatuliwa ndani ya nchi pekee