Magufuli "style" yahamia wilayani Hai, watumishi wafukuzwa kazi

Mkuu wa Wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na wananchi alipofanya ziara katika hosptali teule ya Machame na kuzungumza na wafanyakazi.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
HALMASHAURI ya wilaya ya Hai,mkoani Kilimanjaro, imewasimamisha kazi watumishi wake wanne kwa tuhuma za kughushi hati za mishahara na kughushi nyaraka zilizofanikisha kuchukua jumla ya kiasi cha sh Mil 73.4 zikiwemo fedha za malipo ya muda wa kazi wa ziada kwa madaktari na wauguzi wa Hospitali teule ya Machame.

Tuhuma hizo pia zina mtaja Mweka hazina wa Hosptali hiyo anayedaiwa kushirikiana na watumishi wa halmashauri hiyo kufanya ubadhirifu wa fedha na kwamba tayari Uongozi wa hosptali hiyo iliyo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) dayosisi ya Kaskazini ,umekwisha  mfukuza kazi.

Watumishi wawili kati ya wanne wamesimamishwa kazi kutokana na tuhuma mbili tofauti,moja ni kughushi hati za mishahara,vitambulisho na sahihi za watumishi  waliostaafu  na wengine kuacha kazi na kuchukua mikopo wa Mil 35 katika benki ya CRDB kwa majina ya watumishi walioacha kazi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo