Baada ya kukosa kuingia Bungeni, Balozi Kagasheki atoa ujumbe mzito

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini balozi Khamis Kagasheki ametoa tahadhari kwa baadhi ya watu wanotumia mitandao ya kijamii na kumtuhumu kuwa baada ya kushindwa kupata nafasi ya ubunge ameondoa baadhi ya vitu alivyovitekeleza akiwa mbunge wa jimbo hilo ikiwemo kudaiwa kuondoa mtengo wa radi katika shule ya msingi  kibeta, TV ya wananchi ya uhuru platfom,  gari la kubebea wagonjwa na kuzima umeme katika soko kuu la kashai mjini Bukoba.

Balozi Khamisi Kagasheki ametoa rai hiyo wakati akiongea na waandishi wa habari mjini Bukoba ambapo amesema yeye hakuondoa kitu chochote alichakitekeleza katika jimbo hilo bali hayo nimaneno yanayo enezwa na baadhi ya watu waliopanga kumchafua na kueneza chuku dhidi yake, nahapa anaeleza zaidi. 
 
Balozi Kagasheki amewataka watu wanaotumia nafasi hiyo kumchafua katika mitandao ya kijamii kuacha mara moja kwani hatosita kuwachukulia sheria za kimtandao wale wote wanao diliki kumchafua bila sababu yeyote.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo