Mbunge mteule wa jimbo la Mikumi kwa tiketi ya Chadema Josephu Haule maarufu kama Profesa J amewashukuru wananachi wa jimbo hilo kwa kumpa ridhaa na kuahidi kushirikiana na wananchi wote katika kuleta maendeleo ya jimbo la Mikumi.
Akizungumza na wananchi wa jimbo la Mikumi mbunge huyo mteule Profesa J amesema jimbo la Mikumi lilisahaulika kwa miaka mingi huku wananchi wakiendelea kukosa huduma bora za kijamii ambapo amaesema atahakikisha anaisimamia rasilimali za jimbo la Mikumi ziwanufaishe wananchi wote.
Kwingineko katika jimbo la Morogoro mjini viongozi wa vyama vya upinzani wameeleza kutoridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa madiwani katika kata za Chamwino na mazimbu kutokana na uchaguzi wa kata hizo kugubikwa na changamoto lukuki zikiwemo kuzalishwa vituo feki vya kupigia kura siku ya uchaguzi.