Jimbo la uchaguzi Makete mkoani Njombe tayari limepokea baadhi ya vifaa vya uchaguzi kutoka tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) vitakavyotumika kwa ajili ya kufanikisha uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Akizungumza na mtandao huu wa edwinmoshi.blogspot.com Afisa Uchaguzi wilaya ya Makete Mwl. Gregory Emmanuel (pichani) amevitaja baadhi ya vifaa hivyo kuwa ni pamoja na Tishirts, Mabango, karatasi za mfano za wapiga kura, ambapo mpaka sasa wameshazitawanya kwenye kila kata kwa ajili ya kutoa elimu kwa wapiga kura katika kata za wilaya ya Makete
Amesema kwa sasa tayari elimu inaendelea kutolewa na wananchi wasiwe na hofu na endapo wanahitaji kufafanuliwa mambo mbalimbali wasisite kufika kwenye ofisi za kata zao au makao makuu ya wilaya ili watatuliwe masuala yao
Katika hatua nyingine Mwl. Gregory amewashauri wapiga kura wilayani hapo kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi ikiwemo kuandaa vitambulisho vyao mapema pamoja na kujitokeza kwa wingi kupiga kura
Amesema siku 8 kabla ya uchaguzi mkuu watabandika kwenye kila kituo orodha ya majina ya wapiga kura, hivyo wananchi wawahi waweze kuhakiki majina yao ili wafahamu watakapopigia kura