Nape ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Mtama, Lindi alipata ajali hiyo baada ya tairi la mbele la gari aliyokuwa akiendesha aina ya Toyota Land Cruiser kupasuka na kupinduka mara kadhaa katika eneo la Nyangao mkoani Lindi.
Katika gari hilo, Nape alikuwa peke yake na ndiye alikuwa akiendesha gari hilo ambapo amepata majeraha madogo ila anaendelea vizuri.
Kabla ya ajali hiyo, Nape alikuwa jijini Dar es Salaam ambapo aliungana na mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Pombe Magufuli aliyekuwa na mikutano kadhaa ya kampeni katika jiji la Dar na baada ya shughuli hiyo alikuwa akirejea Lindi kuendelea na kampeni kwenye jimbo lake la Mtama.