Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeshindwa tena kutoa maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kada wa Chadema anayeiomba mahakama hiyo kutoa uamuzi wa kwamba wananchi wanatakiwa kukaa mita ngapi baada ya kupigakura ambapo baadhi ya wananchi wameiomba mahakama hiyo kufanya maamuzi mapema kwani jambo hilo linamasilahi makubwa na taifa.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na jopo na majaji watatu wakiongozwa na jaji Sakieti Kihiyo imekuwa ikifuatiliwa na wadau mbalimbali wakitaka kujuwa nini hatima ya shauri hilo kwani umbali sula la umbali wa upi watu wanapaswa kuka bada ya kupoiga kura umekuwa ni moja ya mambo yanayozungumziwa sana wa wapiga kura akiahirisha shauri hilo kiongozi wa jopo Mh Kihiyo amesema maamuzi yatatolewa tarehe 23 saa nne asubuhi ambapo baadhi ya wananchi waliozungumza nasi wamesema wanaimani kuwa mahakama inachelea kutoa maamuzi kwa sababu inahitaji muda wa kutosha wa kufanya maamuzi haya kwani jambo hilo ni nyeti kwa taifa.
Wengine wameiomba mahakama hiyo kufanya maamuzi hayo mapema kwani muda umekwisha na watanzania wanataka kujuwa nini cha kufanya ili wasije kujikuta wanaingia katika mgogoro na vyombo vya dola.
Katika shauri hilo mlalamikaji Bw Amy Kibatala anatetewa na wakili Peter Kibatala ambapo katika madai yao ya msingi ni kwamba anaiomba mahakama itoe tafsiri ya kifungu namba 104 (1) cha sheria ya uchaguzi sura 343 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2010 kuwa ni umbali gani watu wanatakiwa kukaa kutoka kwenye kituo cha kupigia kura.