Rais Kikwete amewahakikishia watanzania kuwa uchaguzi utakuwa huru na amani

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anayemaliza muda wake Dr Jakaya Kikwete amewahakikishia watanzania uchaguzi utakuwa huru na wa amani na wasiwe na hofu, na kuwaonya wale ambao wanapanga kuleta fujo watakiona.

Rais Kikwete ambaye pia ni mweyekiti wa CCM ametoa tahadhari hiyo hapa Chakechake Pemba wakati akiwahutubia umati wa wanachama wa CCM na wananchi waliofika katika uwanja wa Gombani ya kale katika mkutano wa mwisho kwa Pemba wa kampeni ya mgombea urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya CCM ambapo amesema yeye bado ni amiri jeshi mkuu wa nchi na kuwataka watanzania kwenda kwa wingi kupiga kura.
 
Naye mgombea urais wa Zanziabr Dr Ali Mohamed Shein katika mkutano huo amewahidi wazanzibari kuwa ahadi alizozitoa katika mikutano ya kampeni zake atahakikisha anazitekleza kwa vile yamo ndani ya ilani ikiwa ni pamoja na umarishaji wa miundombinu na kuwapatia sekta ya uvvi vifaa na boti za kisasa.
 
Katika mkutano huo mkubwa wa aina yake kufanyika kiswani Pemba na kuhudhuriwa karibu na viongozi wote wa juu wa SMZ ambapo pia mgombea mwenza wa urais wa mungano Mhe Samiha Suluhu aliwaakikishia watanzania hasa walemavu na wazee kuwa serikali ya CCM itawawekea mazingira mazuri ya maisha yao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo