Chama cha Democratic DP kimeiomba Serikali na vyombo vya dola kufuatilia kwa kina chanzo cha kifo cha mwenyekiti wa chama hicho Mchungaji Christopher Mtikila kufuatia kuibuka utata wa kifo hicho kilichotokea kwa ajali ya gari Octoba NNE mwaka huu
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwa marehemu Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya amesema wameshangazawa na kushtushwa na ajali hiyo na wanafikiri ni ajali ya kupangwa
Naibu Katibu Mkuu wa DP, Abdul Mluya amesema Mchungaji Mtikila alidai kufuatiliwa na gari za aina tofauti tangu alipokuwa akielekea mjini Mwanza kwenye kipindi baada ya kumaliza mikutano mjini Bunda Septemba 25 na 26 mwaka huu .
Hata hivyo ameeleza kusikitishwa kwao na baadhi ya picha zilizopigwa katika eneo la ajali huku wakiwa na maswali mengi juu ya aliyepiga picha hizo.
Mchungaji Patrick Mgaya ambaye alikuwa na marehemu kwenye gari wakati ajali inatokea amesema walikuwa wakifuatiliwa na gari aina ya Toyota Land cruza kutoka Mafinga mpaka ajali ilipotokea.
Mwili wa mchungaji Mtikila umeagwa jana saa 3 asubuhi jijini Dar es salaam katika viwanja vya Karimjee na baadaye ukusafirishwa kupelekwa Ludewa, Njombe kwa mazishi.
Miongoni mwa madai aliyokuwa akidai Mchungaji Mtikila ni pamoja na Tanganyika yake.