Rais Kikwete atoa kauli......ni kuhusu nyumba za NHC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete amewashauri watendaji wa shirika la nyumba kuwa wabunifu kwa kujenga nyumba zenye hadhi ya juu pembezoni mwa mji ili kupunguza msongamano katikati ya jiji  la Dar Es Salaam.

Pia amelitaka shirika la nyumba la taifa kujiunga na mkongo wa taifa ili kuweza kufanya shughuli zake kupitia mtandao na kurahisisha upatikanaji wa  huduma kwa watanzania.

Akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa Morroco Square, ulio chini ya shirika la nyumba la taifa,ambapo katika mradi huo kutakuwa na nyumba za makazi,nyumba za biashara,Ofisi na maeneo ya michezo kwa watoto.

Rais Kikwete amesema  kukamilika kwa mradi huo kunaiweka Tanzania  katika hatua  ya juu  ya maendeleo ya kiuchumi.

Aidha shirika la nyumba la taifa limeiomba serikali kufanya marekebishoa katika sheria ya  kuuza nyumba kwa wananchi ili kutoa fursa kwa watanzania waishio nje na kwa raia kutoka mataifa mbalimbali.

Mkurugenzi wa shirika la nyumba Nehemia Mchechu, amesema mradi huo utakuwa na fursa mbalimbali za kiuchumi na kijamii kwa maendeleo ya watanzania .

Mradi huo wa Morocco Square utaigharimu  billon 150 na unatarajiwa kukamilika kukamilika desemba 2017.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Rais Kikwete amepokea hati za utambulisho wa balozi mteule wa Ubelgiji, Paul katia, Balozi wa Hispania, Felix Costales Artieda na Balozi wa Msumbiji Patricia Clemente.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo