Pengo lililoachwa na Deo Filikunjombe laanza kuonekana Ludewa

Kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo Ludewa hayati Deo Filikunjombe kimeanza kuleta madhara makubwa ndani ya jamii ya wanaludewa kutokana na ukweli usiopingika kuwa alikuwa msaada wa Wanaludewa wengi wakiwemo zaidi ya wanafunzi 700 wa shule za Sekondari ambao walikuwa wakilipiwa ada ya shule kwa pesa zake binasfi.
Akiongea kwa uchungu mkubwa mmoja wa wanafunzi hao Richard Mtweve kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Mavanga alisema kuwa hayati Filikunjombe alikuwa ni msaada mkubwa katika masomo yake na wengine hivyo hana uwezo tena wa kuendelea na masomo yake kwani uwezo wa kujilipia ada haupo.
Richard alisema kuwa nyota ya matumaini kwa wanafunzi zaidi ya mia saba imezimika ghafla kwa kuondokewa na muhimili wa maisha ya Wanaludewa na Watanzania kwa ujumla kwani licha ya kuwalipia ada ya shule wanafunzi pia alitoa misaada mikubwa katika shule zote za msingi na Sekondari wilayani hapa na kusaidia katika majanga mbalimbali likiwemo lile la kuezuliwa kwa Shule ya msingi Ludewa Mjini ambapo alijitolea kukarabati madarasa yaliyobomolewa kwa nguvu zake binafsi kwa kusaidiana na wananchi katika mambo madogomadogo.
Alisema katika shule ya Sekondari Mavanga hayati Filikunjombe aliwasaidia kukarabati dahalia na ujenzi wa baadhi ya madarasa na kuhakikisha wanafunzi anaowalipia ada wanapata mahitaji yote muhimu ya kielimu bila kujali kabila au dini.
Nao vijana wa stendi ya mabasi wilayani Ludewa wameanza kupata ugumu wa maisha mara baada ya kupotelewa na mpendwa wao Filikunjombe  kwani alitoa ajira kwa zaidi ya vijana 100 ambao wengi wao ni bodaboda ya madereva  ambao tayari ajira zao zimeshaingia mgogoro.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo