Utazame "muziki" wa Lowassa mjini Monduli

Mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA Edward Lowassa ameingia mjini Monduli kwa kishindo na kupokelewa na maelfu wa wakazi wa jimbo hilo huku shughuli zikisimama kwa muda,

Miaka 20 iliyopita ilikuwa ni ngome imara ya CCM lakini hii ni Monduli mpyaa kabisa.

Mgombea huyo wa nafasi ya urais Edward Lowassa akiwa mjini Monduli amewaahidi kuhakikisha anakuwa mstari wambele katika kutetea na kuimarisha maendeleo ya wanamonduli na watanzania kwa ujumla.
 
Awali akihutubia mikutano ya hadhara wilayani Monduli katika maeneo ya Ingaruka, Loksari, Makuyuni na Monduli mjini amesema bado ni dhamira yake kuona watanzania wananufaika na rasilimali amabzo zimewazunguka.
 
Akizunguma mara baada ya kukabidhiwa rasm kijiti cha kuwania nafasi ya ubunge Bw Julias Kalanga amemhakikishia Edward Lowassa kuwa atahakikisha anakuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo mjini Monduli.
 
Mgombea huyo wa nafasi ya urais na timu yake ya kampeni ameendelea kupata uungwaji mkono na idadi kubwa ya wananchi ambapo kesho anatarajia kuanza ziara ya kampeni zake mjini Same mkoani Kilimanjaro.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo