Vyama vya siasa vya TLP na CCM vimewataka viongozi wa vyama vya umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) wawaombe radhi watanzania kwa unafiki waliounyesha awali wa kumkashifu mh edward lowasa kuwa ni fisadi na sasa wanamtakasa kuwa ni mtu safi anayefaa kuliongota taifa.
Mwenyekiti wa taifa wa TLP Dr.Augustine Mrema na mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya hai Bw.Amani Uronu wametoa rai hiyo kwa nyakati tofauti walipoongea na waandishi wa habari mkoani Kilimanjaro juu ya mchakato wa uchaguzi unaoendelea nchini.
Dr.Mrema na Bw.Uronu wamesema,kitendo cha viongozi hao kinaua upinzani ndani ya nchi na kuwafanya wapinzani wasieminike kwa kuwa vigeugeu ndani ya jamii.
Kauli hiyo imeungwa mkono na mchungaji Joachim Mmanyi wa kanisa la Pentekoste na kwamba viongozi hao wametenda dhambi ya unafiki dhidi ya Dr.Wilboard Slaa aliyetarajiwa wananchi wampigie kura ya urais na badala yake kumweka mtu aliyetuhumiwa kwa ufisadi.