Hali mbaya Mtera, TANESCO wachukua maamuzi magumu

Shirika la umeme nchini Tanesco limesimamisha uzalishaji wa umeme katika Bwawa la Mtera baada ya mitambo yake kuzimwa katika kipindi cha wiki moja sasa kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo linalozalisha megawati 80 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa kuzalishwa na Bwawa moja hapa nchini.

Meneja wa Tanesco kituo cha kuzalisha umeme cha Mtera mhandisi Abdallah Ikwasa amewaambia waandishi wa habari waliotembelea kituo hicho kujionea hali halisi ya uzalishaji umeme kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kupungua kwa kina cha maji katika Bwawa hilo hata baada ya kituo hicho kulazimika kuzalisha umeme chini ya mita za ujazo zinazoruhusiwa kitaalam.
 
Aidha muhandisi Ikwasa amesema kufuatia hali hiyo Kwasasa Tegemeo pekee la nishati ya umeme ni mitambo ya kuzalisha umeme inayotumia gesi asilia ambayo shirika bado linaendelea na  hatua za uimarishaji vituo vyake kwa lengo la kuondoa adha ya kukatika kwa umeme katika maeneo yaliyounganishwa kwenye gridi ya taifa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo