Aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,Letcia Mosore (katikati)akizungumza na waandishi wa (habari hawapo pichani) juu ya ukiukaji wa katiba ya chama hicho kumvua madaraka iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Mwakilishi NCCR-Mageuzi ,Hamlyn Erasto,Kushoto ni Kamishina Mkoa wa Ruvuma,Mchatta Mchatta.
ALIYEKUWA Makamu Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, Letcia Mosore amesema kuwa taratibu za kumvua nafasi ya makamu mwenyekiti wa chama hicho zilikiukwa kwa mujibu wa katiba yao.
Kukiukwa kunatokana na matumizi mabaya ya madaraka ya mwenyekiti wa chama, James Mbatia kuchukua kikao cha Septemba 22 kufanya tathimini ya uchaguzi ndani ya chama na kuita ni kikao cha kamati ya maadili.
Amesema kuwa kuondolewa kwa nafasi hiyo ni kutokana na kufanya kikao na waandishi wa habari ambapo anadai mwenyekiti wa chama hicho ni kitendo cha kutaka kuhujumu NCCR-Mageuzi.
Letcia ametaka Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia kutaja viongozi anaoshirikiana nao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati mwenyekiti,Mbatia aliteuliwa nafasi nyeti ya ubunge na Rais na Mwenyekiti Chama cha Mapinduzi (CCM),Jakaya Kikwete je ni kazi ni gani aliyoifanyia CCM.
Amesema katika nafasi yake ni kosa la kufanya kikao na baadhi ya viongozi katika hoteli ya Land Mark kutokana na mamlaka ya nafasi yake anaweza kuitisha mkutano mahali popote pale.
Leticia amesema kuwa anaomba taratibu kama ni kweli amekiuka katiba ziainishwe kwa kikao kwa mujibu wa katiba hiyo katika mkutano wa kamati kuu.
Amesema kamati ya maadili hana imani nayo kutokana wajumbe hao kuwa ni sehemu ya ndugu wa mwenyekiti wa chama hivyo wasingweza kutenda haki dhidi yake.