Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chini ya jopo la majaji Lugano Mwndambo, Sekiene Kihiyo na Aloycious Mujulis waliokuwa wakisikiliza kesi inayohusu wananchi kukusanyika umbali wa mita 200 kutoka kituo cha kupigia kura siku ya uchaguzi, imeahirisha kusikiliza kesi hiyo ili kupima hoja zilizotolewa pande zote.
Kesi hiyo imepangwa kuendelea kusikilizwa tena na kutolewa maelekezo hapo kesho.