"Sasa hivi nathubutu kusema kuwa, Lowassa ndiye anafaa kuwa Rais wa Tanzania" - Msigwa

Mbunge wa Iringa Mjini anayemaliza muda wake Peter Msigwa, ameomba radhi kwa kauli aliyowahi kuitoa katika uwanja wa Mwembe Togwa kuwa ‘Atakaye muunga mkono Lowassa akapimwe akili’.
Akizungumza kupitia kipindi cha Panga Pangua cha Azam TV, msigwa amesema ni kweli yeye alitoa kauli hiyo lakini amedai naye ni binadamu na kuna wakati anateleza.
“Ni kweli na nimeipima akili yangu, nimechekecha, nikatafakari na mwisho wa siku nikatambua kwamba kauli yangu niliitoa kimakosa.
Sasa hivi nathubutu kusema kuwa, Lowassa ndiye anfaa kuwa Rais wa Tanzania baada ya Dk Kikwete” alisema Msigwa.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo