Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Pombe Magufuli leo ametoka jijini Mwanza kuingia jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kampeni za lala salama kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika jumapili hii.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl julius Nyerere, Magufuli alikutana na kusalimiana na rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyekuwa akisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea mkoani Ruvuma kuwaaga wananchi wa mkoa huo.
Baada ya hapo Magufuli aliendelea na ratiba yake ya mikutano ya kuomba ridhaa kwa wakazi wa Dar es Salaam. Maeneo amabyo Magufuli amefanya mkampeni leo ni pamoja na Kigamboni katika Uwanja wa Machava, Mbagala Zakhiem, Ubungo Bus Terminal, Ubungo Shekilango, Tandika Mwembeyanga, Uwanja wa TP Sinza na kumalizia mkutano mkubwa katika viwanja vya Biafra.
Akiwahutubia wananchi wa Kigamboni, Magufuli aliwatoa hofu kuwa hakuna atakayedhulumiwa kufuatia ujenzi wa mji wa kisasa katika eneo hilo. pia alisema eneo hilo atalifanya kuwa wilaya mpya ili liwe na hadhi na kupewa huduma zote kama jimbo linalojitawala.
Baada ya kuwa wilaya ataipatia Hospitali ya Wilaya na huduma zingine zitaongezwa.
Akiwa maeneo mengine, Magufuli aliwanadi wabunge na madiwani wanaowania nafasi hizo kwa tiketi ya CCM huku akiwaahidi wananchi kuwaboreshea maisha, kupambana na rushwa na mafisadi.
Pia aliongeza kuwa, daraja la Kigamboni linatarajiwa kukamilika mwezi ujao ambapo wananchi watavuka bure.