Kuhudhuria kwenye mikutano ya kampeni za wagombea ni raha, maana kuna mambo mengi hususan vioja, maneno matamu, vituko na vijembe vya wagombea.
Kwa mfano mgombea ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Sambwee Shitambala (CCM), juzi alitoa kali mbele ya wananchi wa Kata ya Ruanda, aliposema akichaguliwa hawezi kuvaa tena nguo za kijani kwa kuwa atakuwa ni mbunge wa wananchi na siyo chama.
“Niwahakikishie tu wananchi, mchakato wa CCM ulishapita, hivyo watakaonichagua ni wananchi wa Mbeya Mjini. Kwa hiyo mimi sitavaa sare za CCM ofisini na kwenye mikutano yangu ili kutoa fursa sawa,” alisema Shitambala.
Mbali na hilo, alimponda mmoja wa wagombea wenzake katika jimbo hilo akidai ametengeneza kiwanda cha ‘machizi’ ambao kazi yao ni kuzomea tu na kuleta vurugu na maandamano